Sasa kwa vile umempokea Kristo...
Jinsi ya kujua kwamba Yesu yumo maishani mwako.
Sasa, je, umemkaribisha Yesu maishani mwako? Unajuaje?Kwa hiyo yuko wapi sasa? Kumbuka Ufunuo 3:20
Yesu alisema ataingia katika maisha yako. Je, si kweli?
Je, unajuaje kuwa Mungu amesikia ombi lako? Mungu ameahidi kwanba lo lote tuombalo na kuamini litatendeka.
Aliye na Yesu anao uzima wa milele.
"Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu"(1 Yohana 5:11-13).
Umshukuru Mungu kila siku kwamba Yesu anaishi katika maisha yako.
Uwe na hakika kwamba hatakuacha kabisa. (Mathayo 28:20). Amekupa uzima wa milele.
Ukumbusho wa muhimu...
Usiyategemee mawazo ya moyo wako.
Unaweza kujisikia leo unafuraha ndipo kesho ukawa na huzuni. Kwa vyovyote utakavyojisikia Yesu Kristo habadiliki maishani mwako. (Waebrania 13:5).
- Ukweli wa Mungu ndio wenye uwezo wa kutuongoza.
- Tunaunganishwa na uwezo wa ukweli kwa imani.
- Tunapotii ukweli, hali ya kujisikia ya moyo (maoni) huongozwa vyema.
- Tunamtegea Mungu na ukweli wake wala sio hali ya kujisikia ya moyo.
Basi, usitegemee mawazo yako, bali utegemee ukweli wa Neno la Mungu kwa imani.
Kwa kuwa sasa umempokea Kristo
Tangu ulipompokea Kristo mabadiliko mengi yametokea:
- Yesu ameingia katika maisha yako (Ufunuo 3:20).
- Umesamehewa dhambi zako (Wakolosai 1:14).
- Umefanyika kuwa mwana wa Mungu (Yohana 1:12).
- Utazidi kujua makusudi ya Mungu kwa maisha yako (2 Wakorintho 5:14,15,17).
Je, unafikiri kuna jambo lililo bora kuliko kumpokea Yesu katika maisha yako?
Basi, labda ungependa kumshukuru Mungu sasa kwa vile alivyokurehemu.
Tunathibitisha imani yetu tunapomshukuru Mungu kwa maombi.
Tuombe tukiwa huru.
Na sasa je?
Juinsi ya Kukua Kiroho
Kama mtoto mchanga unahitaji kukua, utaendelea vizuri katika maisha ya kiroho ukiyafuata mashauri yafuatayo kila siku:
- Zungumza na Mungu kwa maombi (Yohana 15:7).
- Soma Neno la Mungu (Matendo 17:11).
- Uwe mwaminifu kwa Mungu (Yohana 14:21).
- Mshuhudie Kristo kwa matendo yako na maneno yako (Mathayo 4:19 na Yohana 15:8).
- Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako
(1 Petro 5:7). - Umruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-18 na Matendo 1:8).
Ni muhimu kwa Wakristo kushirikiana
Biblia inatuambia kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25).
Ebu, tutumie mfano wa moto. Kuni nyingi zikilundikwa pamoja zinawaka vizuri sana, lakini ukiuondoa ukuni mmoja na kuuweka peke yake utapoa. Vile vile wewe haifai kuishi maisha ya kikristo peke yako.
Ukishirikiana na watu wengine ambao wamempokea Yesu kuwa Mwokozi wao utazidi kuwa na moto wa imani.
Uhudhurie kanisa ambapo watu wanaiamini Biblia kuwa ni kweli na Yesu anatukuzwa.
Vifaa maalum vilivyopo kwa ajili ya kukua Kikristo.
IIwapo umekuja kwa Kristo kibinafsi kupitia wasilisho hili la Injili, vifaa vitakavyo kusaidia kukua Kikristo vinapatikana kwa ajili yako.Kwa habari zaidi, kamilisha fomu ifwatayo au andikia LIFE Ministry, S.L.P. 62500-00200, NAIROBI, KENYA.