Je, Umesikia Juu Ya Kanuni Nne Za Kiroho?
1. Mwenyezi Mungu ANAKUPENDA, naye anataka kukupangia mpango wa ajabu kwa maisha yako.
(Kumbukumbu zilizoko kwenye ukurasa wa mtandao huu zimetoka katika Biblia na zinafaa kusomwa katika muktadha popote iwezekanapo.)
Upendo wa Mungu
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele" (Yohana 3:16).
Mpango wa Mungu Kwako
[Yesu asema] "Mimi nilikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele" (Yohana 10:10).
Je, kwa nini watu wengi hawana uzima huo?
Ni kwa sababu . . .
2. Mwanadamu ni mwenye DHAMBI. Dhambi zake zimemtenga na Mungu. Kwa hiyo hajui upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yake.
Mwanadamu Ni Mwenye Dhambi
"Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23).
Mungu alimwumba mwanadamu kwa kusudi la kushirikiana naye, lakini mwanadamu alikwenda kinyume cha mpango wa Mungu. Alichagua kumwasi Mungu badala ya kumtii. Kumwasi Mungu ni kufanya dhambi. Mtu anapoishi kinyume cha mapenzi ya Mungu anaendelea kuishi maisha ya dhambi.
Mwanadamu Ni Mwenye Dhambi
"Lakini maovu yenu imewatenga ninyi na Mungu wenu"
(Isaya 59:2).
Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi. Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa njia nyingi: dini, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi.
Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu...
3. Yesu Kristo ni njia ya PEKEE ya kuondoa dhambi. Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu.
Alikufa Ili Atulete Kwa Mungu
"Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu" (1 Petro 3:18).
Yesu Yuhai
"Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko" (1 Wakorintho 15:3,4).
Yesi Ndiye Njia Ya Pekee
"Yesu akamwambia, 'Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi" (Yohana 14:6).
Mwanadamu peke yake hawezi kushirikiana na Mungu. Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na tena awe daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa Mungu.
Sasa kanuni ya nne itakuambia jinsi uwezavyo kumjua maishani mwako...
4. Inakupasa KUMPOKEA Yesu awe Mwokozi na Mtawala wako. Ndipo utajua upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yako.
Unampokea Kristo Kwa Imani
"Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake"(Yohana 1:12).
"Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu" (Waefeso 2:8,9).
Tunapompokea Kristo, Tunapata Kuzaliwa Upya
(Soma Yohana 3:1-8.)
Inakupasa Kumkaribisha Yesu Maishani Mwako
[Yesu asema] "Tazama, nasimama mlangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake . . ." (Ufunuo 3:20).
Kumpokea Yesu Kristo ni:
- Kujua wewe ni mwenye dhambi na kumgeukia Mungu na kutubu.
- Kumtegemea Mungu akusamehe.
- Kumkaribisha Yesu Kristo atawale maisha yako kwa imani ili uwe kama anavyopenda.
�
Je, ni picha gani iliyo mfano wa maisha yako?
Je, ni picha gani ambayo ungependa iwe mfano wa maisha yako?
Yafuatayo ni maelezo ya jinsi uwezavyo kumpokea Kristo ndani ya maisha yako?
Unaweza kumpokea Kristo sasa
(Sala ni kuzungumza na Mungu)
Mungu anaufahamu moyo wako. Yafuatayo katika sala hii yanaweza kukusaidia kumpokea Kristo ukiomba kwa moyo wa kweli:
"Bwana Yesu Kristo, ninakuhitaji, mimi ni mwenye dhambi. Nimekubali kwamba nimejitawala maisha yangu mwenyewe, na kutengana nawe. Asante kwa kifo chako msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na kwa kunisamehe zote. Sasa nageuka na kutubu. Bwana, nakuomba uingie ndani ya maisha yangu na kunitawala kabisa. Badili maisha yangu yawe kama upendavyo wewe. Amin.."
Je, sala hii ni sawa na haja ya mayo wako?
Kama sala hii ni sawa haja ya moyo wako, basi omba sasa na umkaribishe Kristo aingie maishani mwako.
Sasa kwa vile umempokea Kristo...